Thursday, June 17, 2010

BUSTANI ZA DAR ES SALAAM


Wapenzi wa bustani na mazingira, tunapotembelea miji mingi tunaona jinsi gani miji inavyoweza kubadilishwa kwa kutengeneza bustani zenye hadhi zinazoangaliwa na kutunzwa.
Jiji kama Dar es salaam lina kila uwezo wa kutengeneza bustani za maua mbali mbali hasa yale yasiyohitaji maji kwa wingi na yale hanayostawi kwenye hali ya joto na jua kali.
Pamoja ya kwamba miti na maua yanapandwa pembeni ya barabara lakini,watu hawajali kutunza na kutoa elimu ya kuzuia uharibifu usio na lazima. Elimu itolewe kwa wadau wa sehemu zilizopandwa maua na miti, ili wajue umuhimu wa mimea hiyo

Sheria zitungwe na kutumika kwa wale ambao watavunja sheria hizo. Pawekwe adhabu kali,kwa wanaoegesha magari kwenye bustani za katikati ya barabara. Watembea kwa miguu wawekewe sehemu mwafaka za kupita bila kubugudhi bustani.Hapa tuangalie sehemu ambayo haitamchosha mtembea kwa miguu, kwani kama njia za wapita kwa miguu zitakuwa mbali na zenye mzunguko basi watu watakatiza na kupita kwenye bustani.

Jiji limetenga fedha kwa ajili ya kutunza jiji,lakini ufuatiliaji wa karibu unatakiwa kuongezeka.
Meya wa JIJI la Dar es salaam,Tunakutegemea wewe kuonyesha wadau kuhusu mazingira bora. Tunaona ni vyema sehemu ya jangwani bonde la Msimbazi lipandwe mimea inayostahili na kuitunza. Usisahau ulinzi wa misitu ni muhimu pia,kwani usipolinda wataishi vibaka. Mfano mdogo ni miti iliyopandwa pale barabara ya Morocco kati ya kinondoni na Magomeni hakuna ulinzi kwahiyo kuna uhalifu wa kila namna.

No comments:

Post a Comment