Tuesday, June 1, 2010

MIMEA



Binadamu wameumbwa kuwa na mapenzi mbalimbali ya vitu vinavyokuwa katika maisha ya kila siku. Wengine wanapenda sauti mbali mbali(Music), wengine wanapenda kuwa na wanyama aina mbalimbali,wngine wanapenda michezo,n.k.

Mimi napenda mimea hasa inayostawi ndani na nje.Mimea ya bustani iliyopandwa chini ya ardhi au ile iliyo kwenye vyombo vya kupandia maua. Napenda mimea inayotoa maua ya kuvutia na ile ambayo inavutia hata bila maua.

Mimea inayotuzunguka ni kati wa vitu tunavyoishi navyo bila kufikiria umuhimu wake. Ni kawaida kwa binadamu kuona mimea mbalimbali ikiwa katika mazingira yetu.
Mimea hiyo inaweza kuwa kwenye njia ya kuelekea nyumbani kwako,bustanini,ndani ya nyumba, makanisani n.k.tunaiona kila siku,wakati mwingine bila hata kifikiria wala kutambua kuwa ipo.Lakini ikondolewa lazima utaona kuwa kumekosekana kitu fulani

Wakati mwingine unaikwanyua,unaikanyaga, inainmwagia hata sumu, unaikata wakati unapita au kwa makusudi tu unaiondoa kabisa bila sababu.Mimea hii inaweza kuwa midogo sana,mikubwa yaani miti au midogo inayoweza kutengeneza vichaka vidovidogo.

Hebu tufikirie kama mimea tunayoiona ingekuwa ina uwezo wa kuonyesha au kusema mateso yanayoipata kutoka kwa binadamu, ikaamua kueleza hadharani au kufanya maandamano pangekuwa hapatoshi, dunia ingekuwa ndogo. Hata hao viongozi wa nchi wasingeweza kukemea. Ingeweza kusema binadamu angejiona kiummbe msumbufu mharibifu,asiyejali uhai wa viumbe wengine woliohai.

Mimea ina maombile mbali mbali ili kuweza kuhimili mikimikiki ya dunia. Inajaribu kujilinda kwa njia nyingi kama vile:
Kuwa na miba mikali
Kuwa na vimelea vinavywasha ukivigusa
Kutoa harufu mbalimbali ambazo adui anaweza kuona kuwa ni harufu mbaya
Ukubwa au udogo wa umbo lake unaweza kuwa kinga kwake
Sehemu mmea unakostawi kama vile kwenye miamba na misitu mikubwa ili kuwa mbali na usumbufu wa binadamu au wanyama wengine n.k.

Mimea imeumbwa hivyo ili binadamu mwenyewe aipende,aitumie , ailinde kama ilivyo.
Tuitunze mimea inayotuzunguka kwani faida zake ni nyingi kuliko tunavyofikiria.Mmea kama pambo ni burudani tosha inaongeza hadhi ya sehemu, iwe nyumba, hoteli, ofisi, makabuni n.k. Mimea inatumika kama dawa,inasafisha hewa chafu ya dunia n.k.

Je mimea tunayoishi nayo tunaifahamu majina? Unaweza kupata mgeni akiwa anapita kwenye bustani yako akavutiwa na mmea ambao kila siku uko nao lakini akiuliza jina ukashindwa kujibu. Vilevile ikiwa unajua jina la mmea unaoutunza ni rahisi kujua na tabia yake na mazingira yanayofaa kuupanda.Pamoja na kuwa kuna vitabu vingi vinavyoonyesha majina mbalimbali hasa ya kisayansi lakini unaweza usipate jina la mmea ambao uko bustanini kwako. Majina ya kisayansi ni magumu kutamka na kuyakariri, lakini unaweza kupatia majina ya kikabila, au mahali ulipopatia mmea,au sura ya ule mmea,sehemu unapopenda kuota n.k.

Wadau hebu tutoe picha za mimea na majina yake kama tunavyoyajua.
Tuelezane tabia na namna tunavyoweza kutuza mimea mbalimbali
Tupeane changamoto ili tupende mazingira yanayotuzunguka
Wadau tutoe maoni yetu Kwa Lugha ya kiswahili au Kiingereza

No comments:

Post a Comment